Info
Wapendwa Taifa la Mungu,
Tunayo furaha kubwa kuwakaribisha katika Jimbo Katoliki Moshi Online Tv. Hiki ni chombo kwa ajili ya kuinjilisha kujibu hitaji la msingi la nyakati. Mababa Watakatifu na Mitaguso mbalimbali imedokeza umuhimu wa kutumia vyombo vya kisasa kwa ajili ya Uinjilishaji kwani huleta faida kwa binadamu na kutoa mchango mkubwa katika uinjilishaji (Inter Mirifica 2).
Lengo msingi la chombo hiki ni kuinjilisha na kuwa mfano bora wa kutoa habari kwa usahihi, Lengo hili linafungamana na lengo la Mamlaka Funzi ya Kanisa ya kufundisha, kutakatifuza na kuchunga wanakanisa. Hivyo Kanisa linapata mahala sahihi na salama pa kufundishia.
Sehemu ya kwanza ya Uinjilishaji katika Jimbo Katoliki Moshi ilikua ana kwa ana kuanzia 1890 mpaka miaka ya 1970. Sehemu ya pili ilikua Uinjilishaji kwa njia ya Jumuiya Ndogo ndogo za Kikristo ambapo uinjilishaji ulijikita katika kuimarisha na kutembelea familia, Sehemu ya tatu ya Uinjilishaji ilijikita katika kutumia vyombo vya kisasa.
Stats
Joined Invalid Date
0 total views