Chaneli hii ilianzishwa kwa lengo la kujifunza maisha ya watakatifu. Tumeumbwa tuwe watakatifu. Maisha ya mkristo yanapaswa yaendane na matakwa ya Mungu katika kuishi utakatifu. Kupitia channel hii utajifunza kutoka kwa watakatifu ili uweze kuishi vyema lengo la kuwa Mkristo, yaani kuishi katika muungano na Mungu ukiuchuchumilia utakatifu.